23. Naye Daudi alipouliza kwa BWANA, alisema, Usipande; zunguka nyuma yao, ukawajie huko mbele ya miforsadi.
24. Kisha itakuwa, hapo utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo nawe ujitahidi; kwa maana ndipo BWANA ametoka mbele yako awapige jeshi la Wafilisti.
25. Ndivyo alivyotenda Daudi, vile vile kama BWANA alivyomwagiza; naye akawapiga Wafilisti toka Geba hata ujapo Gezeri.