23. Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.
24. Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu;
25. na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi;
26. na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi;
27. na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi;
28. na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi;
29. na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;
30. na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi;
31. na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi;
32. na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani,
33. mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari;
34. na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;