2 Sam. 22:42-49 Swahili Union Version (SUV)

42. Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa;Walimwita BWANA, lakini hakuwajibu.

43. Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi,Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.

44. Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu;Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa;Watu nisiowajua watanitumikia.

45. Wageni watanijia wakinyenyekea;Kwa kusikia tu habari zangu,Mara watanitii.

46. Wageni nao watatepetea,Watatoka katika ngome zao wakitetemeka.

47. BWANA ndiye aliye hai;Na ahimidiwe mwamba wangu;Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;

48. Naam, Mungu anipatiaye kisasi,Na kuwatweza watu chini yangu,

49. Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu;Naam, waniinua juu yao walioniinukia;Waniponya na mtu wa jeuri.

2 Sam. 22