39. Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama;Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.
40. Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita;Umenitiishia chini yangu walioniondokea.
41. Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.
42. Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa;Walimwita BWANA, lakini hakuwajibu.
43. Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi,Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.
44. Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu;Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa;Watu nisiowajua watanitumikia.
45. Wageni watanijia wakinyenyekea;Kwa kusikia tu habari zangu,Mara watanitii.
46. Wageni nao watatepetea,Watatoka katika ngome zao wakitetemeka.
47. BWANA ndiye aliye hai;Na ahimidiwe mwamba wangu;Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;
48. Naam, Mungu anipatiaye kisasi,Na kuwatweza watu chini yangu,
49. Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu;Naam, waniinua juu yao walioniinukia;Waniponya na mtu wa jeuri.
50. Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa,Nami nitaliimbia jina lako.
51. Ampa mfalme wake wokovu mkuu;Amfanyia fadhili masihi wake,Daudi na mzao wake, hata milele.