34. Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu;Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35. Ananifundisha mikono yangu vita;Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.
36. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;Na unyenyekevu wako umenikuza.
37. Umezifanyizia nafasi hatua zangu,Wala miguu yangu haikuteleza.
38. Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza;Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.
39. Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama;Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.
40. Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita;Umenitiishia chini yangu walioniondokea.