31. Mungu njia yake ni kamilifu;Ahadi ya BWANA imehakikishwa;Yeye ndiye ngao yaoWote wanaomkimbilia.
32. Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA?Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?
33. Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu;Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.
34. Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu;Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35. Ananifundisha mikono yangu vita;Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.
36. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;Na unyenyekevu wako umenikuza.
37. Umezifanyizia nafasi hatua zangu,Wala miguu yangu haikuteleza.
38. Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza;Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.