25. Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu;Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
26. Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhiliKwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;
27. Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu;Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.
28. Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa;Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili.
29. Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA;Na BWANA ataniangazia giza langu.
30. Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi;Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.