2 Sam. 22:22-29 Swahili Union Version (SUV)

22. Maana nimezishika njia za BWANA,Wala sikumwasi Mungu wangu.

23. Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu;Na kwa habari za amri zake, sikuziacha.

24. Nami nalikuwa mkamilifu kwake,Nikajilinda na uovu wangu.

25. Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu;Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.

26. Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhiliKwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;

27. Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu;Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.

28. Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa;Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili.

29. Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA;Na BWANA ataniangazia giza langu.

2 Sam. 22