17. Alipeleka kutoka juu, akanishika;Akanitoa katika maji mengi;
18. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,Na wale walionichukia;Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
19. Walinikabili siku ya msiba wangu;Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.
20. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi;Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
21. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu;Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.
22. Maana nimezishika njia za BWANA,Wala sikumwasi Mungu wangu.
23. Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu;Na kwa habari za amri zake, sikuziacha.
24. Nami nalikuwa mkamilifu kwake,Nikajilinda na uovu wangu.
25. Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu;Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
26. Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhiliKwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;