Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa walizozileta kusanyiko ikawa ng’ombe waume sabini, kondoo waume mia, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.