Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.