2 Nya. 17:12-18 Swahili Union Version (SUV)

12. Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina.

13. Naye alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda; na watu wa vita, watu mashujaa humo Yerusalemu.

14. Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, maakida wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa mia tatu elfu;

15. na wa pili wake Yehohanani akida, na pamoja naye mia mbili na themanini elfu;

16. na baada yake Amasia mwana wa Zikri, aliyejitoa kwa BWANA kwa moyo, na pamoja naye mia mbili elfu, watu mashujaa;

17. na wa Benyamini; Eliada mtu shujaa, na pamoja naye mia mbili elfu wenye nyuta na ngao;

18. na wa pili wake Yehozabadi, na pamoja naye mia na themanini elfu waliojiweka tayari kwa vita.

2 Nya. 17