2 Nya. 15:9-14 Swahili Union Version (SUV)

9. Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.

10. Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa.

11. Wakamchinjia BWANA siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng’ombe mia saba, na kondoo elfu saba.

12. Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta BWANA, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote;

13. na ya kwamba ye yote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, kwamba ni mwanamume au mwanamke.

14. Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa mapanda, na kwa baragumu.

2 Nya. 15