15. Ndipo wakapiga kelele watu wa Yuda; ikawa, watu na Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.
16. Wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao.
17. Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli mia tano elfu, watu wateule.
18. Ndivyo walivyotiishwa wana wa Israeli wakati ule, wakashinda wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea BWANA, Mungu wa baba zao.
19. Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang’anya miji, Betheli na miji yake, na Yeshana na miji yake, na Efroni na miji yake.
20. Wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha BWANA akampiga, akafa.
21. Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita.
22. Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.