2 Kor. 7:14-16 Swahili Union Version (SUV)

14. Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.

15. Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu na kutetemeka.

16. Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.

2 Kor. 7