Basi wakarudi, wakampasha habari. Akasema, Hili ndilo neno la BWANA, alilolinena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya, Mtishbi, kusema, Katika kiwanja cha Yezreeli mbwa wataila nyama ya Yezebeli.