2 Fal. 3:1-2 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili.

2. Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA; ila si kama baba yake na kama mama yake; maana akaiondoa ile nguzo ya Baali aliyoifanya baba yake.

2 Fal. 3