Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa BWANA, na matako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa BWANA, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.