17. Naye Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda akaishi baada ya kufa kwake Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli miaka kumi na mitano.
18. Basi mambo yote ya Amazia yaliyosalia, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?
19. Wakafanya fitina juu yake katika Yerusalemu, naye akakimbia mpaka Lakishi, lakini wakatuma watu kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.
20. Wakamleta juu ya farasi; naye akazikwa huko Yerusalemu pamoja na babaze katika mji wa Daudi.
21. Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, aliyekuwa mwenye umri wa miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa baba yake Amazia.
22. Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze.
23. Katika mwaka wa kumi na tano wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda Yeroboamu mwana wa Yehoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala katika Samaria; akatawala miaka arobaini na mmoja.
24. Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA; wala hakuyaacha makosa yote ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.
25. Yeye akaurudisha mpaka wa Israeli toka kuingia kwa Hamathi hata bahari ya Araba, sawasawa na neno la BWANA, Mungu wa Israeli, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii, aliyekuwa wa Gath-heferi.
26. Kwani BWANA akayaona mateso ya Israeli, kwamba yalikuwa machungu sana; maana hakukuwa na mfungwa wala asiyefungwa, wala msaidizi kwa ajili ya Israeli.
27. Wala BWANA hakusema ya kwamba atalifuta jina la Israeli litoke chini ya mbingu; lakini akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
28. Basi mambo yote ya Yeroboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, na jinsi aliyvopigana, akawapatia tena Israeli Dameski na Hamathi, iliyokuwa kwanza ya Yuda, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?