1 Tim. 4:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2. kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3. wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

1 Tim. 4