8. Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.
9. Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10. bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11. Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
13. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.