1 The. 5:3-12 Swahili Union Version (SUV)

3. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4. Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

5. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

6. Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

7. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

8. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.

9. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;

10. ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.

11. Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.

12. Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;

1 The. 5