1 The. 5:19-24 Swahili Union Version (SUV)

19. Msimzimishe Roho;

20. msitweze unabii;

21. jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;

22. jitengeni na ubaya wa kila namna.

23. Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

24. Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.

1 The. 5