1. Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.
2. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
3. Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4. kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5. si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.