Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA.