25. Basi ikawa hivyo tangu siku ile na baadaye; akaiweka iwe amri na agizo la Israeli hata leo.
26. Basi Daudi alipofika Siklagi, aliwapelekea wazee wa Yuda, rafiki zake, sehemu ya nyara, akasema, Angalieni, zawadi yenu katika nyara za adui za BWANA;
27. yaani, kwa hao wa Betheli, na kwa hao wa Ramoth-Negebu, na kwa hao wa Yatiri;
28. na kwa hao wa Aroeri, na kwa hao wa Sifmothi, na kwa hao wa Eshtemoa;
29. na kwa hao wa Rakali, na kwa hao wa miji ya Wayerameeli, na kwa hao wa miji ya Wakeni;
30. na kwa hao wa Horma, na kwa hao wa Korashani, na kwa hao wa Athaki;
31. na kwa hao wa Hebroni, na kwa hao wa kila mahali alipozoelea Daudi mwenyewe na watu wake.