1. Naye Hana akaomba, akasema,Moyo wangu wamshangilia BWANA,Pembe yangu imetukuka katika BWANA,Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
2. Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA;Kwa maana hakuna ye yote ila wewe,Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
3. Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo;Majivuno yasitoke vinywani mwenu;Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa,Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
4. Pinde zao mashujaa zimevunjika,Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.