7. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,Jiwe walilolikataa waashi,Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8. Tena,Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.
9. Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10. ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.