1. Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
2. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
3. ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
4. Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.