10. Na katika makuhani; Yedaya, na Yehoyaribu, na Yakini;
11. na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;
12. na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri;
13. wakuu wa mbari za baba zao; pamoja na ndugu zao; watu elfu na mia saba na sitini; watu wenye ustadi waliofaa sana kwa kazi ya huduma ya nyumba ya Mungu.
14. Na katika Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari;
15. na Bakbakari, na Hereshi, na Galali, na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu;
16. na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.
17. Na katika mabawabu; Shalumu, na Akubu, na Talmoni, na Ahimani, na ndugu zao; naye Shalumu alikuwa mkuu wao;
18. ambao tangu hapo walikuwa wakingojea penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa wangojezi wa rago la wana wa Lawi.
19. Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa mbari ya babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ungojezi wa malango ya maskani; na baba zao walikuwa wamesimamia matuo ya BWANA, wakiyalinda maingilio;
20. naye Finehasi, mwana wa Eleazari, alikuwa mkuu wao hapo zamani, naye BWANA alikuwa pamoja naye.
21. Zekaria, mwana wa Meshelemia, alikuwa bawabu mlangoni pa ile hema ya kukutania.
22. Hao wote waliochaguliwa kuwa wangojezi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyoamaniwa.
23. Basi watu hao na wana wao walikuwa na usimamizi wa malango ya nyumba ya BWANA, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.
24. Hao wangojezi walikuwapo pande zote nne, kuelekea mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini.