1. Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.
2. Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika hozi zao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
3. Na huko Yerusalemu walikuwa wakikaa baadhi ya wana wa Yuda, na wana wa Benyamini, na wana wa Efraimu na Manase;
4. Uthai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imli, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
5. Na wa Washiloni; Asaya, mzaliwa wa kwanza, na wanawe.
6. Na wa wana wa Zera; Yeueli, na ndugu zao; watu mia sita na tisini.
7. Na wa wana wa Benyamini; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;