5. na Gera, na Shufamu, na Huramu.
6. Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi;
7. na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi.
8. Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara.
9. Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu;
10. na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao.
11. Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali.
12. Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake;
13. na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi.