1 Nya. 8:4-18 Swahili Union Version (SUV)

4. na Abishua, na Naamani, na Ahoa;

5. na Gera, na Shufamu, na Huramu.

6. Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi;

7. na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi.

8. Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara.

9. Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu;

10. na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao.

11. Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali.

12. Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake;

13. na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi.

14. Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi;

15. na Zebadia, na Aradi, na Ederi;

16. na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria.

17. Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi;

18. na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali.

1 Nya. 8