25. na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki.
26. Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia;
27. na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu.
28. Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu.
29. Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka;
30. na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali, na Nadabu;
31. na Gedori, na Ahio, na Zekaria,