11. Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali.
12. Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake;
13. na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi.
14. Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi;
15. na Zebadia, na Aradi, na Ederi;
16. na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria.
17. Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi;
18. na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali.
19. Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi;
20. na Elienai, na Silethai, na Elieli;
21. na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema.
22. Na Ishpani, na Eberi, na Elieli;
23. na Abdoni, na Zikri, na Hanani;
24. na Hanania, na Elamu, na Anthothiya;
25. na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki.
26. Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia;
27. na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu.
28. Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu.
29. Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka;