1 Nya. 8:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu;

2. na wa nne Noha, na wa tano Rafa.

3. Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi;

4. na Abishua, na Naamani, na Ahoa;

5. na Gera, na Shufamu, na Huramu.

6. Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi;

7. na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi.

1 Nya. 8