1 Nya. 7:9-20 Swahili Union Version (SUV)

9. Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu ishirini elfu na mia mbili.

10. Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari.

11. Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.

12. Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.

13. Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shilemu; wana wa Bilha.

14. Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;

15. naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.

16. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.

17. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.

18. Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.

19. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.

20. Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;

1 Nya. 7