1 Nya. 7:29-32 Swahili Union Version (SUV)

29. na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.

30. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera.

31. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.

32. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua.

1 Nya. 7