26. na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama;
27. na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.
28. Na hizi ndizo hozi zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;
29. na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.
30. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera.
31. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.
32. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua.
33. Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti.
34. Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.
35. Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali.
36. Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra;
37. na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera.
38. Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara.
39. Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia.
40. Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.