1 Nya. 7:24-31 Swahili Union Version (SUV)

24. Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.

25. Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani;

26. na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama;

27. na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.

28. Na hizi ndizo hozi zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

29. na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.

30. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera.

31. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.

1 Nya. 7