15. naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.
16. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.
17. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18. Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.
19. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.
20. Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;
21. na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng’ombe zao.
22. Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji.
23. Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu mna mabaya nyumbani mwake.
24. Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.
25. Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani;