13. Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shilemu; wana wa Bilha.
14. Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;
15. naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.
16. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.
17. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18. Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.
19. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.