68. na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake;
69. na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake;
70. na katika nusu-kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi.
71. Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;
72. na katika kabila ya Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake;
73. na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake;