49. Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu.
50. Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua;
51. na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia;
52. na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu;
53. na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi.
54. Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza;