40. mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya;
41. mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido;
42. mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;
43. mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
44. Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;
45. mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia;
46. mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri;
47. mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48. Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu.
49. Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu.