24. na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli.
25. Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi.
26. Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu;
27. na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana.
28. Na wana wa Samweli; Yoeli, mzaliwa wa kwanza, na wa pili Abia.
29. Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza;
30. na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.
31. Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe.
32. Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao.
33. Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;
34. mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;
35. mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;
36. mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;
37. mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora;
38. mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.