1 Nya. 6:15-19 Swahili Union Version (SUV)

15. na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.

16. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

17. Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.

18. Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.

19. Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao.

1 Nya. 6