1 Nya. 6:13-23 Swahili Union Version (SUV)

13. na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria;

14. na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;

15. na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.

16. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

17. Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.

18. Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.

19. Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao.

20. Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima;

21. na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai.

22. Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;

23. na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri;

1 Nya. 6