12. na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu;
13. na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria;
14. na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;
15. na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.
16. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
17. Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.
18. Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
19. Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao.
20. Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima;
21. na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai.
22. Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;