10. na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)
11. na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;
12. na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu;
13. na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria;
14. na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;
15. na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.
16. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
17. Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.
18. Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.